
Uaminifu Katika Majukumu Madogo – Mtihani Mkubwa wa Maisha.
"Uaminifu katika majukumu madogo ni daraja la mafanikio makubwa. Jifunze kwa kina jinsi uaminifu unavyojenga tabia, huleta fursa, hujenga amani ya moyo, na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii yako….”

Uaminifu kwa Watu Wengine: Msingi wa Mahusiano na Maendeleo.
Jifunze jinsi uaminifu kwa malengo yako binafsi unavyoweza kubadilisha maisha yako kifedha, kimaadili na kiroho. Gundua faida halisi za kushikilia ahadi ulizojiwekea

Jinsi Uaminifu Unavyoweza Kuleta Mafanikio ya Kweli Katika Maisha.
“Jifunze kwa undani jinsi uaminifu unavyoweza kuwa hatua muhimu ya ukuaji wa kibinafsi, kifedha, na kimaadili...”

Hatua 3 Muhimu Kuanza Kufanikiwa Maishani.
“Jifunze hatua tatu muhimu zinazoweza kukusaidia kuacha maisha ya kushindwa na kuanza safari ya mafanikio ya kweli. Tambua nguvu ya mawazo, maamuzi, na matendo yako kila siku”

Kustaafu Ni Mwanzo Mpya siyo Mwisho
Ni mzee aliyeamua kuanza kuishi ndoto yake kwa kuanza mazoezi ya kujenga mwili akiwa na umri wa miaka 87.Ni mwanariadha aliyeshikilia rekodi ya ushindi wa mbio za mita 400 na 600 katika kundi la watu wa umri wake.Alishikilia rekodi za ushindi 4 mbili nchini Uingereza za dunia katika umri wa miaka zaidi ya 90. Ni mwandishi wa kitabu cha "Age is Just Numbers" alichokiandika akiwa na umri wa miaka 95.

Kama Una Tabia Hii Unasaidia Wengine Kuishi.
Kwa nini mtu mmoja anafanikiwa kumiliki muda wake na kuweza kuonyesha matunda ya namna alivyotumia muda wake vizuri na wakati huo huo mwingine anahangaika namna ya kutawala na kutumia muda wake vizuri?
WATU wengi wanajua kwamba muda ni mali ingawa matendo wanayofanya hayaonyeshi kuunga mkono imani hiyo, na imani bila matendo ni sawasawa kabisa na mtu asiyeamini bado kitu chochote.

Namna Ya Kushinda Tabia Ya Kuahirisha Mambo
Azimio la kujenga makazi ya kudumu ili kuepuka maumivu yanayosababishwa na hali ya majira kubadilika lilipitishwa tangu enzi za mababu na mababu, lakini limeahirishwa mpaka leo. Siyo babu wala baba zake waliofaulu kutimiza azma ya kujenga makazi ya kudumu.
Jitihada za kujikinga na kukinga watoto wake dhidi ya mvua kali iliyokuwa inanyesha wakati mwingine ziligonga mwamba na kujikuta kila mmoja katika familia ya manyani akihangaika kujitafutia namna ya kujizuia na mvua kali iliyokuwa inanyesha.

Maisha Ni Mradi Wako Mwenyewe!
“Maisha ni mradi wa kufanya wewe mwenyewe (life is a do yourself project)” ni msemo na nukuu ya Napolion Hill kupitia kitabu chake maarufu cha Think and Grow Rich alipokuwa anasisitiza juu ya umuhimu wa kila binadamu kutimiza wajibu wake kuhakikisha anafikia kusudi la kuwepo kwake hapa duniani.

Kwa Nini Wengi Hushindwa Kuishi Ndoto Zao!
Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayejua anachotaka kufanya ambaye huthubutu kufanya bila woga na yule ambaye yeye licha ya kujua anapashwa kufanya nini lakini anakosa ujasiri kufanya kwa kuongozwa na hali ya hofu na kusitasita.

Kazi Ni Nyingi, Ajira Chache!!
Ingawa watu wengi wanajua kuwa ulimi huumba na mara nyingi kinywa hukiri kile kinachoujaza moyo,hawaachi kukiri na kujitamkia misemo ambayo imezoeleka katika maisha yao na matokeo yake wanaanza kuiishi. Miongoni mwa misemo hiyo ni pale unaposikia watu wanakiri kuwa hakuna kazi siku hizi na kwa kuwa ndivyo wanavyoamini basi,hivyo ndivyo inavyokuwa kwao na nafasi za kazi zinakuwa adimu kweli kweli.

Namna Nzuri Ya Kutafuta kazi
Hakuona sababu ya kubweteka kwa sababu alikuwa anatoka katika familia tajiri,badala yake alipita mtaani kutafuta kitu cha kufanya bila kujali kwamba yeye ni msomi wa chuo kikuu aliyehitimu katika fani ya uchumi na utawala.

Maneno Bila Matendo Haitoshi!
“Nitalima maharage mengi sana na mahindi katika shamba hili.Siku ya kuuza mazao yangu hakuna mkulima mwingine atakayepata nafasi ya kuuza,kuanzia asubuhi mpaka muda wa kufunga soko nitauza mazao yangu tu” alisisitiza

Muhimu Ni Mwisho Siyo Mwanzo!
Kuna mafundi wengi vijana na watu wazima waliopita mikononi mwake ambao wale waliotimu kufuata maelekezo yake kwa kufanya kazi kwa ubora wa wa hali ya juu, uaminifu na kujituma ilimtofautisha sana na mafundi wengi wa aina yake kijijini kwao na maeneo yaliyozunguka kijiji chao.

Kitu Hiki Kila Mtu Anacho!!!
Kuna kitu kimoja pekee hapa duniani ambacho Mungu amempa kila mtu bila upendeleo ni muda. Kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa mtu kunategemea sana namna anavyotumia muda wake.

Namna Ya Kupata Fursa Ya Biashara
Watu wengi wanatamani kuwa wajasiliamali lakini changamoto kubwa inayowakwamisha ni kutokua na uwezo wa kubuni wazo la biashara.Watu wanaofanikiwa kila watakakokwenda ni wale wenye uwezo wa kutazama tofauti na watu wengine wanavyotazama na kupata fursa katikati ya kile wengine wanachoita matatizo.

Jifunze Kusema Hapana Itakusaidia…
Jifunze kusema hapana mahali unapopaswa kusema hapana na ndio mahali unapopaswa kusema ndiyo.Kamwe usijaribu kusema ndiyo wakati moyoni mwako unajua kabisa ulipaswa kusema hapana na kadhalika usiseme ndiyo mahali ambapo ulipaswa kusema hapana.

Usidharau Mwanzo Mdogo
Kila kazi au biashara unayotaka kufanya ni muhimu kukumbuka kwamba unahitajika angalau uwe na maarifa ya msingi ya kukuwezesha kufanya biashara hiyo.Maarifa hayo yanaweza kuwa umeyapata kutoka shuleni au hata kutokana na uzoefu wa muda fulani ukifanya au ukimsaidia mtu.Maarifa yanakuwezesha kujua mazuri na mabaya yaliyo ndani ya fursa hiyo ya kufuga kuku.Kipengenere hicho ukikiruka unaweza ukapata hasara kwanza kabla ya kuingia kupata faida.

Madhara Ya Mtazamo
Ikiwa unataka kufanikiwa katika eneo lolote maishani mwako unapaswa kwanza kujifunza namna ya kufikiri vizuri,kwa sababu pengo kati ya watu waliofanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa,lipo katika namna wanavyofikiri (mtazamo)

Tofauti Ya Kazi Na Wito
Umewahi kujiuliza kuna tofauti gani kati ya wito na kazi? Ingawa watu wengi wanachanganya maana ya maneno haya mawili muhimu katika maisha na kujikuta wanazungumzia wito mahali pa kazi na kuzungumzia kazi mahali pa wito,ipo tofauti kubwa kati ya kazi na wito.

Badili Uchungu Kuwa Wito
Umewahi kumsamehe mtu aliyekukosea bila kuangalia ukubwa wa kosa alilokufanyia hata kama anaendelea kukukosea?. Mwezi wa pili mwaka 1993 Marry Johnson alipokuwa kazini alipokea simu yenye taarifa mbaya ikimjulisha kuhusu kifo cha mwanaye wa pekee Laramiun Bry ambaye alikuwa ameuawa kikatiri na muuaji Oshea Israel huko nchini Marekani.