Jifunze Kusema Hapana Itakusaidia…
Picha kwa hisani ya mtandao.
Jifunze kusema hapana mahali unapopaswa kusema hapana na ndio mahali unapopaswa kusema ndiyo.Kamwe usijaribu kusema ndiyo wakati moyoni mwako unajua kabisa ulipaswa kusema hapana na kadhalika usiseme ndiyo mahali ambapo ulipaswa kusema hapana.
Katika kitabu cha Think and Grow Rich cha mwandishi maarufu Napolion Hill anasema, nanukuu: “life is a do yourself project” mwisho wa kunukuu. Tafsiri yake kwa Kiswahili anamaanisha “maisha ni mradi wa kufanya wewe mwenyewe” Maisha ni mradi wako binafsi,unaopaswa kuutekelezwa na wewe kwa muda maalum bila kuweka visingizio vya namna yoyote.
Karibu tena msomaji wa makala zetu kwenye mtandao wetu. Leo nimechagua kukushirikisha mada inayoitwa “JIFUNZE KUSEMA HAPANA” na nikushukuru tu kwa muda wako uliotenga uendelea kufuatilia mada hizi. Nathamini sana mchango wako huo.
Kama maisha ni mradi wa kufanya mwenyewe basi, hakuna anayepaswa kumsaidia mwingine kuhakikisha anatekeleza mradi wake kulingana na jinsi alivyopewa na Mungu.Unabuni mwenyewe,unaandika na kupanga mwenyewe,unatekeleza mwenyewe na siku ya kumaliza mkataba wako wa maisha utawajibika kwa aliyekuumba wewe mwenyewe.
Inakadiriwa kuwa dunia yetu kwa sasa ina idadi ya watu zaidi ya 7.6+ bilioni na kama hujui tumegawanyika katika makundi mawili makubwa:kundi la wale wanaoishi maisha yao na wale wanaoishi maisha ya watu wengine. Wanaoishi maisha yao ni wale ambao wanajua wanachopaswa kufanya hapa duniani na wale wanaoishi maisha ya wengine ni wale wasiojua kile wanachopaswa kufanya hapa duniani matokeo yake wanasaidia watu wengine kukamilisha miradi yao,au kwa lugha rahisi wanasaidia watu wengine kuishi! Hii ni ngumu kumeza ee!
Mimi na wewe ni waratibu wa miradi yetu wenyewe na tutawajibika kwa matokeo yoyote tutakayosababisha kwa kipindi tulichopewa na Mungu kuishi msimu huu unaoitwa maisha,kumbuka wote tumepewa rasilimali sawa kabisa kukutuwezesha kutekeleza mradi wako bila kujali uko wapi,una rangi gani wala una hali yako.
Maisha ni msimu mfupi sana hivyo tunapaswa kuwa waangalifu kuhakikisha tunatumia kwa usahihi kipindi hicho kifupi na kwa wakati sahihi,huwezi kuwa mratibu wa kila kitu unapaswa kuchagua kitu kimoja au vitu vichache utakavyotumia kwa uaminifu msimu huu wa maisha nab ado ukafikia mafanikio.
Watu wengi wanadhani kuwa na vitu vingi vya kufanya ndiyo njia ya kukusaidia kufanikiwa katika mambo mengi,apana watu waliofanikiwa wanaandama vitu vichache na kuhakikisha wanatekeleza kwa ufanisi mkubwa huku wakiwa wanafunzi wa kitu hicho kila siku.
Ili uishi maisha yako kwa ufanisi ni muhimu sana kuwa na maono na kujua kusudi la kuwepo hapa duniani; kwako kwa nini? Kwa sababu hakuna hatari kubwa ya kuogogopwa duniani inayoweza kusababisha maafa makubwa kama mtu kuishi bila maono. Kuishi bila maono ni sawa sawa na mtu anayekwenda safari bila kujua anakoelekea mtu huyo hawezi kufika anakotaka kufika kwa sababu hata njia ya kumfikisha huko haijui.
Ni muhimu sana kusema hapana pale inapopasa kusema hapana na hii ni kwa manufaa yako wewe mwenyewe. Usijarib kuishi ili ufurahishe watu wanaokuzunguka kwa sababu hakuna sehemu ya wao kuwajibika kwa maisha yako kwa vyovyote vile. Kufanya hivyo siyo udhaifu bali kuna nguvu kubwa kwenye kusema hapana ili kuokoa muda wako ambao umeratibiwa kwa kazi na muda maalum hapa duniani.
Unahitaji kuwa na uwezo kusema hapana ndani mwako ili uweze kuwa na ujasiri wa kusema hapana kwa nje bila kujali dunia inavyokuchukulia.Kama huna uwezo ndani mwako kujiambia hapana hutaweza kabisa kusema hapana kwa nje.
Sema hapana kujiridhisha mwenyewe kwanza wala usitafute kuridhisha watu wengine.Sema hapana pale fursa zisizoshabihiana na kusudi la kuwepo kwako usije kujikuta unaingia kwenye mkumbo wa kutumikia kusudi la mtu mwingine ambalo huna wajibu nalo mahali popote.
Ipe nafsi yako uhuru na furaha ya kusema hapana kwa fursa mbalimbali za watu zinazokuja kwa sura ya kusaidia jamii kumbe zinataka watu wa kusaidia makusudi ya watu fulani kuwepo hapa duniani yaweze kutimia.
Usisite kutamka hapana inapokuja mialiko ambayo hukutegemea wala haiko katika mpango wako wa siku,wiki,mwezi na mwaka kwa sababu huwezi kuwa maratibu wa kila kitu.Zipo fursa ambazo unapaswa kuzikataa ili kufuata maono yako.
Usiogogope kusema hapana kwa watu wanaokuja kwa sura ya kutaka kukusaidia kumbe wenyewe ndio wenye uhitaji mkubwa wa msaada wako ili waweze kutimiza maono na malengo yao kupitia mlango wa nyuma.
Kwa nini watu wengi wanaona ugumu kusema hapana? Je wote wanaosema ndio wanamaanisha ndiyo kweli? Kuna watu wengi ambao wanatamka maneno vinywani mwao ambayo hayawakilishi shauku na ukweli ulio ndani mwao.
Je kusema hapana kunapunguza mahusiano na watu au kunayaongeza? Ni heshima kubwa kusema hapana ukimaanisha hapana maana utaweza kuishi unachosema kuliko kusema ndiyo halafu ukashindwa kuishi maneno yako. Sema hapana,ndiyo nasema sema hapana mahali pa kusema hapana.
Sema hapana nasema tena sema hapana ale inapobidi usiseme ndiyo ili kufurahisha watu maana maisha yako hayana mtu mwingine wa kundai. Nataka nimalizie kwa kukuuliza swali hili muhimu kama tulikuwa pamoja na nakusudia mjadala mkubwa kuibuka. Je unaishi maisha yako au unaishi maisha yatu wengine?
Naamini kuna kitu utakuwa umejifunza kupitia Makala hii fupi ya “Jifunze Kusema Hapana”. Ikiwa ungependa kusoma zaidi makala zetu endela kutembelea mtandao wetu. Na kama ungependa kuingia kwa undani katika mada hizi kwa maswali au kujifunza zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu,kupiga au whatsapp kupitia simu hapo chini.
Ni mimi rafiki na kocha
Ni mimi rafiki na kocha Philipo Lulale
Simu +255784503076
Email:maishanifursa2017@gmail.com