Namna Nzuri Ya Kutafuta kazi
Kazi
Hakuona sababu ya kubweteka kwa sababu alikuwa anatoka katika familia tajiri,badala yake alipita mtaani kutafuta kitu cha kufanya bila kujali kwamba yeye ni msomi wa chuo kikuu aliyehitimu katika fani ya uchumi na utawala.
Aliwashukuru wazazi wake kwa malezi mazuri na elimu waliyompa hadi kufikia ngazi ya shahada ya pili ya chuo kikuu na kwa upande mwingine alijua jukumu lililokuwa limebaki lilikuwa ni la kwake yeye mwenyewe kutafuta kazi itakayomsaidia kutoa mchango wake hapa duniani.
Karibu tena katika makala zetu za kujenga katika mtandao wa maishanifursa.com. Kwanza nikushukuru sana kwa kuendelea kutuamini na kufuatilia kazi zetu. Kazi hii ina maana tu kwa sababu wewe upo. Kama ni mara yako ya kwanza kusoma makala zetu nikukaribishe kwa mikono miwili na kuahidi kuwa hutakaa ujute kuufahamu mtandao huu.
Usikubali kuimba wimbo wa hakuna kazi
Hakuna wakati hata mmoja katika maisha yetu itafikia nafasi za kazi zisiwepo kabisa. Kinachotokea ni upungufu wa nafasi zenyewe usiyolingana na ongezeko la watu wanaotafuta ajira. Ukweli ni kwamba nafasi za kazi zipo ila kwa watu maalum wanaoziona.
Ukiamua kutafuta kazi jitahidi kushinda kule kazi zinakopatikana kwani kazi haitakufuata nyumbani kukuambia kuwa unahitajika. Lazima ujue kuwa nafasi za kazi kwa watu waliokaa tu hazipo, nafasi zilizopo ni za watu wabunifu na wanaojituma. Lakini watakujuaje kama utakuwa unashinda nyumbani? lazima kuwepo na mahali pa kuanzia.
Ukweli ni kwamba watu wanatafuta nafasi za kazi na nafasi za kazi zinatafuta watu wa pekee kwa ajili ya kujaza mapengo yaliyo wazi.Hata nafasi zingine zilizo na watu zinatafuta watu watu sahihi kutokana na kwamba wanazalisha chini ya matarajio ya waajiri wao na hili ni tatizo kubwa katika jamii inayotuzunguka.
Wimbo wa hakuna kazi ni dhana na maoni ambayo siyo uhalisia. Kazi zilizobakia zinatafuta watu wabunifu wanaoweza kujitofautisha na watu wengine. Watu wanaoweza kutazama hadi nje ya pazia na kuona fursa mahali ambapo wengine wanaona haiwezekani kuwepo fursa.
2. Toka nyumbani
Alitembelea kila alikosikia kuna nafasi ya kazi na kupeleka maombi lakini hakufanikiwa kupata kazi mapema kwa kuwa waliokuwa wanatafuta kazi ni wengi katika zama hizi ambazo wahitimu wanaoingia kwenye soko la kazi ni wengi kuliko nafsi mpya katika soko la ajira.
Siku moja akiamua kubadilisha mbinu za kuomba kazi,badala ya kupeleka maombi ya kazi kwa kuandika barua na kupelekea CV alichagua kampuni ambayo alikuwa anatamani kufanya kazi kwenye kampuni kubwa ya kufua vyuma na kuwahi kila siku kwenye lango kuu.
Alijua kwamba yeye kama mchumi angesaidia sana kampuni hiyo kukua lakini nani alikuwa anamjua mpaka amwitie kazi akiwa nyumbani! Kwa hiyo alijua kuwa yeye ni mgeni katika kazi na hakuna aliyekuwa anajua mchango anaoweza kutoa.
3. Nenda kazi zinakopatikana
Kila siku asubuhi alijihimu kwenda katika lango kuu la kuingilia na kuungana na vibarua wengine ambao wangelikuwa wanabahatisha kama watapata nafasi ya kufanya kibarua chochote ili mradi mkono uende kinywani.
John hakuwa na shida yoyote katika familia yake angeweza kupata kila ambacho angehitaji kupata,lakini kilichomsumbua ilikuwa ni alihitaji kuwa na kitu ambacho wakati wa uzee wake ataonyesha kuwa hiki kimetokana na ubunifu wake badala ya kutegemea mali za wazazi pekee yake.
Ingawa alikuwa hajaajiliwa. lakini namna ya ufanyaji kazi wake ilimtofautisha kabisa na vibarua wengine na kujikuta uongozi unaanza kumpenda na kujua. Aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa na uongozi wa kampuni ulianza kutambua na kuona mchango wake aliokuwa anatoa katika kampuni.
Hakuchagua kazi alifanya kila alichokuwa anatumwa,kuanzia kazi za kufanya usafi,kubeba mizigo kutoka pointi moja kwenda nyingine,kutumwa huku na huku,alifanya bila kinyongo chochote.Katika kikao cha uongozi waliamua kumpa John ajira ya mkataba wa mwezi mmoja mmoja kama msimamizi wa vibarua.
4. Onyesha uwezo wako wote
Siku moja Mungu alitaka kumwinua John kupitia kisa cha mgomo mkali uliotokea hapo kiwandani.Wafanya kazi walikuwa wameistisha mgomo mkubwa wa kkudai maslahi yao na kuondolewa unyanyasaji ambao walidai kufanyiwa wafanya kazi wa chini.
Uongozi wa kiwanda ulishindwa kabisa kutatua mgogoro huo,hata uongozi wa serikali uliingilia kati bila mafanikio,wafanya kazi walikataa kata kata kusikiliza chochote bila kutekelezewa mahitaji yao,nao ni kama walishindwa.
John aliamua kuingilia kati kwanza kuongea na viongozi wa chama cha wafanya kazi kiwandani hapo ambao baada ya maongezi marefu aliwaomba wamruhusu japo dakika 10 aongee na wafanya kazi walio katika mgomo.Alipewa nafasi na kuongea na wafanyakazi kuwaomba wasifanye uharibifu wowote wa mali za kiwanda kwani hasara haingekuwa ya kiwanda tu.
Ilibainika John alikuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi na ndipo sasa alienda upande wa uongozi aliwaomba yeye awe msuluhishi wa mgogoro huo.Wengine walimbeza na wengine walishauri asihukumiwe kabla hajapewa kazi hiyo,walimpa kazi ya kusuluhisha.
Kazi ya John ilikuwa ni kuuonyesha uongozi tatizo kubwa ambalo walikuwa nalo katika mfumo wao na kwamba yeye alikuwa na dawa ya kuweza kumaliza tatizo hilo.Kwa kuwa kampuni haikuwa na namna tena ya kumaliza mgogoro huo alianza kazi ya kujitolea kusaidia menejimenti kuondokana na hilo tatizo na ndani ya wiki moja alikuwa amefanikiwa kumaliza mgogoro huo,mazungumzo kati ya uongozi wa kiwanda na wale wa wafanya kazi yalifanyika na kufikia muafaka.
Kuanzia hapo bodi ya waakurugenzi ilitaka kumjua zaidi John ni nani na kampuni iliamua kumwajiri mara moja kama meneja msaidizi wa kiwanda baada ya kugundua John alikua na shahada ya pili ya maswala ya uchumi na u
Maisha ni fursa bila mipaka ,siku zote jiulize ni kitu gani kitakachomshawishi mwajiri yeyote akuajiri wewe na kumwacha mwingine.Kila mtu anahitaji ufunguo wa fursa zake ili aweze kufungua na kutimiza kusudi la kuwepo kwake hapa duniani.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala kitu kingine kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha yako usisite kuwasili nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo. 15,June 2017.
Ni mimi rafiki na kocha Philipo Lulale
WhatsApp: +255784503076-
Email: maishanifursa2017@gmail.com