Kuanzia Ulipo: Njia Kuelekea Kuishi Ndoto Zako.

UCHACHE WINGI WA PESA SIYO KIGEZO

Umewahi kujiuliza kwa nini mtu mmoja anabaki kulalamika na kushindwa kuanza kuishi ndoto zake kwa kisingizio cha kutokuwa na pesa ya kutosha, wakati huo huo kuna mtu anaanza kuishi ndoto yake kwa kutumia mazingira na pesa kama hiyo hiyo mwenzake anayoita ndogo?

Hujawahi kukuta mtu amejibatiza kwamba yeye hana kitu yaani anashindwa kuanza kuishi maisha yake kwa kusubiri mpaka atakapokuwa na rasilimali za kutosha ingawa hana hata mpango wa kuziongeza hizo rasilimali anazosubiri? Mtu anasuburi miezi, miaka inapita bila kuwa na tumaini lolote huku akitumia pesa anayoita ndogo kila siku?

Je ni kweli kuna watu waliopendelewa na wengine hawakupendelewa? Au kuna watu wana bahati na wengine hawana bahati? Au kuna watu waliopewa rasilimali nyingi na wengine wamenyimwa na kupewa pungufu?,au kuna mabara, nchi na maeneo ambayo Mungu ameyapa upendeleo maalum ndiyo maana wapo wanaofanikiwa kuishi ndoto zao? na je wale wanaoshindwa kabisa kwa sababu walikozaliwa ni miongoni mwa maeneo yaliyokosa upendeleo wa Mungu?

Ni kitu gani kinachowatofautisha watu hawa wawili wanaoishi katika dunia moja, mmoja anafanyq kitu kwa kutumia mazingira na rasilimali ndogo zilizopo na mwingine anashindwa kabisa kuanza chochote anachotqka kwa kuamini kuwa hana rasilimali za kutosha? Kumbuka wakati huo huo mtu anaosema hana rasilimali anaendesha maisha pengine na familia yake kila mwaka hajawahi kuacha kutumia rasilimali  hizo kwa matumizi ya maisha lakini imani yake zinatosha kwa kula na basi siyo kwa mambo makubwa!.

Je dunia tunayoishi imeumbwa kwa namna ambayo kuna mahali sifa yake ni upungufu na pengine pana sifa ya utoshelevu wa kila kitu mtu anachohitaji ili kutekeleza chochote anachotaka kufanya? Haijalishi unakaa wapi wala una hali gani, wala rangi au hali yako,bali dunia inaongozwa na kanuni ambazo zinaiongoza ili mradi mtu yeyote mahali popote, akizifuata dunia inatoa kile mtu anachohitaji na zikivunjwa basi dunia haitoi kile ambacho mtu anataka maana kuna kanuni imevunjwa.

Kama dunia inaongozwa na kanuni za maisha basi watu wengi wako katika adhabu ya vifungo mbalimbali kulingana na ukubwa wa makosa waliyofanya bila kujalisha kama mtu ana taarifa au hajui kinachoendelea. Nguvu ya ujumbe niliobeba ambayo ninashirikisha watu kila ninapopata nafasi kwa yeyote ninaekutana naye kupitia kazi zangu ni kufundisha binadamu wenzangu makosa niliyowahi kufanya ili waweze kukwepa kufanya yale ambayo mimi na wengine kama mimi tulifanya ili safari yao ya mafanikio iwe fupi na hapo nitakuwa nimeongeza thamani katika maisha ya binadamu wenzangu,kuwatendea haki na kutimiza wajibu wangu muhimu.

Hiki ni kitu nikichoishi bila kujua kama kina gharama na madhara makubwa kwa maisha yangu mwenyewe. Mimi ni mhanga wa eneo hili kabla sijajua na kuanza kuishi maisha yangu,rasimali nyingi zimepita mikononi mwangu na kushindwa kuzitumia kuanza kuishi ndoto na maisha yangu kwa kuamini uongo kwamba ni ndogo hazitoshi kunifanya niishi maisha yangu. Kwa mtazamo huo nilichelewa sana kuanza kuishi maisha yangu kosa ambalo msomaji wangu singependa urudie kukifanya.

Haina maana yoyote ya watu wengine kutangulia duniani kama watu wazima tuliopitia uzoefu mwingi wa kushinda na kushindwa tutaacha vijana na wengine wanaotaka kuishi maisha yao warudie makosa ambayo sisi tulikwisha kufanya hapana tutakuwa hatuwatendei haki kabisa. Kutokuielewa dunia inavyofanya kazi ni changamoto ambayo imekwaza watu wengi sana kuanza kuishi ndoto na maisha yao.Dunia yenyewe tangu ilipoumbwa haijawahi kupungukiwa na chochote, ipo tayari kutoa chochote mtu atakachotaka ili mradi amefuata au amevunja kanuni. Habari njema ni kwamba mtu asipofuata kanuni anapata majibu na akifuata kanuni kadhalika anapokea sawa na alivyoomba.

Kutokuielewa dunia inavyofanya kazi ndicho chanzo cha matatizo mengi ikiwemo wahamiaji haramu ambao wanakamatwa kila siku wakijaribu kutorokea nchi za nje kwa imani kwamba katika nchi zao za asili hakuna fursa ya kuishi maisha yao kwa hiyo afadhali hata wangekuwa wanyama wanaoishi labda nchi za magharibi kuliko kuishi huku ambako hakuna namna yoyote ya mtu kuendelea. Usiseme pesa haitutoshi semi pesa hainitoshi kwa sababu kipimo unachopimia wewe siyo lazima kifanane kwa mwingine kutumia kipimo hicho unachopimia wewe. Kila nchi kuna watu tajiri wanaoishi maisha yao bila mipaka na masikini wa kutupa wanaolala katika mitaro.

Ngoja nihitimishe makala yangu kwa kukusisimua kidogo na kipande hiki ili ufunguke kama ulikuwa bado unaona kila kitu kinachopita mkononi mwako hakitoshi. Shida kubwa ya watu wengi ni kutokujua tofauti kati ya mbegu na mavuno kwa hiyo wanakula mpaka mbegu.

Wakati hiyo laki moja inayopita mikononi mwako mara kwa mara na kuishia kuila kwa sababu unaona haitoshi, kuna mtu anatafuta elfu 50 siku akiishika basi safari yake ya mafanikio inaanza. Wakati wewe unatamani kupata milioni 3 kuna mwenzako hiyo ni hela ya kumpa mama kwenda kufanya manunuzi sokoni maana yeye ana mipango ya kuanzia milinoni 100 na kuendelea. Wakati mtu mmoja anatafuta milioni kuanzia 100 ili aanze kuishi maisha yake, kwa mwingine mipango yake ni kuanzia bilioni na kuendelea.

Kuna mtu sasa hivi ukimpelekea fursa ya milioni 100 hafanyi maana anasubiri apate fursa ya mamilioni ya pesa hiyo milioni 100 ni kama unamchezea tu. Maisha hapa duniani ndivyo yalivyo kila mtu anacho kipimo chake mwenyewe cha kujipimia kadri ya umbali anaotaka mtu kufika. Hakuna pesa inayotosha wala pesa isiyotosha tatizo la watu wengi ni mitazamo waliyojiwekea wenyewe bila kujua na wala siyo uchache wa rasilimali pesa.

Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao kwao pesa imekuwa haitoshi kila siku, basi makala hii iwe ni wito wa kukusaidia kuvuka na kujikwamua kutoka katika mtengo huo ulijiviriga m wenyewe. Watu wenye mitazamo ya kufanikiwa hawasubiri mpaka wawe na pesa wanayoita nyingi ndipo waanze kuishi ndoto zao za muda mrefu. Kumbuka ukiendelea kusubiri wazo linalolia ndani mwako siyo mali yako ni mali ya Mungu aliyeliweka ndani mwako ili aweze kuwahudumia waja wake kupitia wewe. Ukiendelea kusubiri bila kubadilisha wazo lilo ndani mwako basi mwenye wazo ataliondoa na kumpatia mtu mwingine mwenye utayari wa kuweka kwenye matendo kile anacho waza. Hujawahi kukuta mtu mahali fulani anaon mwenzake kaanzisha biashara halafu anashika kichwa: “Aisee nilikuwa na wazo hili muda mrefu sasa mwenzangu yeye kaazisha”

UNAHANGAIKA KWA MUDA MREFU KUTEMBEA NA WAZO LA BIASHARA AMBALO UMESHINDWA KULITEKELEZA KWA KISINGIZIO CHA KUTOKUWA NA PESA NYINGI! USISITE KUWASILIANA NASI TUKUSAIDIE. TUTAKUONGOZA KUTOKA WAZO HADI KUANZA KUISHI NDOTO YAKO.

Previous
Previous

Anzia Pale Unapoweza.