“Nguvu Ya Imani Katika Kila Unalofanya”

Nguvu ya imani katika kila unalofanya.

Je, unakumbuka kuwa dunia tunayoishi inaongozwa na kanuni na sheria zilizowekwa? Sheria hizi, kama sheria nyinginezo zilizotungwa na binadamu, zinasimamia mstakabali wa maisha duniani, na zisipofuatwa, wakiukaji hukabiliwa na adhabu.

Kuna msemo unaosema kila kitu unachokiona kimeumbwa mara mbili. Kwanza, katika ulimwengu wa (roho) ulimwengu wa kufikirika ule usioweza kuonenkana kwa macho na ulimwengu halisi ule unaoonekana kwa macho. Vitu vyote unavyoona leo ambavyo havikuumbwa moja kwa moja na Mungu, ni matokeo ya mawazo ya watu wakati fulani. Hakuna kinachoonekana leo ambacho hakikuwa wazo mwanzoni.

Majumba tunamoishi, magari tunayopanda, ndege, meli, mashamba makubwa, ranchi za wanyama, biashara kubwa na ndogo - vyote hivi ni matokeo ya mawazo ya watu waliyokuwa nayo wakati fulani. Bila shaka, umesikia au unajua kuhusu hiki kitu kinachoitwa mtazamo (mindset). Nataka nikukumbushe umuhimu wa mtazamo ili kufanikiwa katika maeneo mbalimbali ya maisha yako.

Kuna mambo manne muhimu unayopaswa kujua, ikiwemo hiki kinachoitwa mtazamo. Kufanikiwa au kutokufanikiwa katika jambo lolote kunategemea sana mtazamo ulionao katika maisha yako. Mzunguko wa mambo huanza na mtazamo (mindset), uamuzi (decisions), matendo (actions), na matokeo (results). Vitu hivi vinategemeana na inategemea sana mtazamo wako ulivyo.

Mtazamo huhamasisha uamuzi, na uamuzi huhamasisha matendo. Matendo huhamasisha matokeo, na mwisho matokeo huhamasisha mtazamo.

Ikiwa mtazamo wako ni hasi, basi uwe na uhakika kwamba utachukua uamuzi hasi, matendo na matokeo yatakuwa hasi, na mwisho wa siku mzunguko huo unaweza kuwa kazi zaidi.

Kadhalika, mtazamo chanya itapelekea uamuzi chanya, matendo yatakuwa chanya, na hakuna atakayezuia matokeo kuwa chanya. Mwisho wa siku, matokeo hayo yataweza kuhamasisha fursa na mtazamo chanya. Kumbuka, akili yetu inavyofanya kazi imegawanyika katika sehemu mbili, yaani, conscious na subconscious mind. Conscious mind ni pale tunapofanya mambo tukiwa na ufahamu wa kinachoendelea, na subconscious ni pale tunapofanya kitu bila kuwa na taarifa ya kile kinachoendelea.Hata hivyo kuna sehemu muhimu sana ya akili ambayo haisemwi sana na watu wengi na hii ni “super conscious mind” au akili ya Mungu. Katika hizo tatu akili kubwa na muhimu ni akili ya Mungu. Hii ndiyo minayofanya mtu afanye mambo makubwa ambayo hata kwa akili ya kawaida yanaweza kuonekana kama hayawezekani. Akili nyingi ya mtu bila kuwepo akili ya Mungu itakuwa na mapungufu mengi katika kufanya maamuzi. Tunahitaji akili ya Mungu katika kila jambo tunalofanya.

Wataalam wanasema binadamu anatumia sehemu ya ubongo wake ya conscious mind kwa 10% tu na sehemu iliyobaki ya subconscious mind inachukua 90%.

Kwa kuwa na mtazamo chanya na kutumia nguvu ya imani katika kila unalofanya, unaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha yako na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na ulimwengu kwa ujumla. Endelea kufanya kazi kwa bidii na kuamini katika uwezo wako, na hakuna kitakachokuwa haiwezekani kwako.
Ikiwa unajambo lolote ambalo ungependa tukusaidie ili uweze kuvuka kutoka ulipo kwenda mahali pengine, usisite kuwasiliana nasi kwa kubofya kitufe hapo chini.

Previous
Previous

Jifunze Kupitia Makosa.

Next
Next

Safari ya Ndoto: Dr. Kakenya Anayeishi Maono Yake.